Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Chad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Chad inahusu eneo la Afrika ya Kati ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Chad.

Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni ya ziwa Chad.

Katika historia kabla ya ukoloni, mara nyingi wakazi wa kaskazini, ambao ni Waarabu au walioathiriwa na utamaduni wao, waliwapiga vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.

Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.

Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.

Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Idriss Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Chad kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.