Historia ya Jamhuri ya Kongo
Mandhari
Historia ya Jamhuri ya Kongo inahusu eneo la Afrika ya Kati ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Kongo.
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo.
Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi waliotawala eneo lote na kuendesha biashara katika beseni ya mto Kongo.
Baadaye eneo hilo lilikuwa sehemu ya koloni la Afrika ya Kiikweta ya Kifaransa
Baada ya uhuru tarehe 15 Agosti 1960 nchi ilitawaliwa na Wakomunisti tangu mwaka 1970 hadi 1991.
Kuanzia mwaka 1992 zilifanyika chaguzi kwa mfumo wa vyama vingi, lakini mwaka 1997 vilitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Rais Denis Sassou Nguesso ametawala miaka 26 kati ya 36 yamwisho.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Jamhuri ya Kongo kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |