Historia ya Burkina Faso

Historia ya Burkina Faso inahusu eneo la Afrika ya Magharibi ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Burkina Faso.
Historia ya awali
[hariri | hariri chanzo]Wawindaji-wakusanyaji waliishi nchini kuanzia miaka ya 14000 KK hadi 5000 KK hivi. Kilimo kilianza miaka 3600 KK - 2600 KK.
Wamossi, Wafulani na Wadyula walivamia eneo hilo katika karne ya 8 hadi karne ya 15 BK.
Kuanzia karne ya 11 Wamossi waliunda falme kadhaa, muhimu zaidi ukiwa ule wa Wagadugu.
Koloni la Wafaransa
[hariri | hariri chanzo]Nchi ilianzishwa na Wafaransa kwa njia ya kugawa koloni la Kodivaa mwaka 1919. Jina la koloni jipya lilikuwa Volta ya Juu (kwa Kifaransa: Haute Volta), kutokana na mto Volta unaoanzia huko.
Kati ya miaka 1932 na 1947 eneo lake lilitawaliwa na makoloni ya jirani.
Baada ya uhuru
[hariri | hariri chanzo]Tangu mwaka 1960 nchi ikawa huru.
Kiongozi wa nchi Thomas Sankara alibadilisha jina la nchi tarehe 4 Agosti 1984 kuwa Burkina Faso, yaani nchi ya watu waadilifu (kwa lugha ya Kimossi).
| Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Burkina Faso kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |