Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Morisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Morisi inahusu visiwa vya Bahari ya Hindi mkabala wa Afrika Mashariki ambavyo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Morisi.

Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.

Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.

Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon.

Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.

Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi.

Nchi ilipata uhuru tarehe 12 Machi 1968, ikawa jamhuri tarehe hiyohiyo mwaka 1992.

Mnamo Oktoba 3, 2024, serikali ya Uingereza na Mauritius ilitangaza, katika tamko la pamoja, uhamisho wa hiari wa visiwa vya Chagos kwenda Mauritius. Kisiwa cha Diego Garcia, ambako kambi ya kijeshi ya Camp Justice iko, ndicho pekee katika mkataba huu mpya, huku utawala ukikabidhiwa kwa Uingereza na serikali ya Mauritius kwa kipindi cha angalau miaka 99. Mnamo Mei 22, 2025, Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer alitia saini makubaliano rasmi ya uhamisho huo. Chini ya masharti ya makubaliano, atoli ya kimkakati ya Diego Garcia na eneo lake la buffer la kilomita 38 vilirejeshwa mara moja Uingereza. Mkataba huo unaruhusu kuendelea kwa kazi ya msingi wa pamoja wa Uingereza na Marekani katika kisiwa hicho kwa miaka 99 ijayo, na kuongezwa kwa miaka 40 na haki inayofuata ya kuondolewa kabla. Mauritius itapokea malipo ya kila mwaka ya pauni milioni 165 kutoka Uingereza kwa miaka mitatu ya kwanza, ikifuatiwa na pauni milioni 120 kwa mwaka katika miaka kumi ijayo. Baada ya hapo, malipo haya ya kila mwaka ya pauni milioni 120 yatawekwa kwenye mfumko wa bei.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Morisi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.