Bunduki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Askari na bunduki
Aina mbalimbali za bunduki

Bunduki ni silaha inayorusha risasi dhidi ya shabaha yake. Ndani ya bunduki inatokea mlipuko wa baruti na gesi joto za mlipuko zinasukuma risasi kuelekea mwendo wa kasiba yake. Kutokana na sifa hii huitwa pia silaha ya moto.

Bunduki ya kisasa huwa na akiba ya ramia katika chemba yake isipokuwa silaha kadhaa za kuwinda. Silaha za kijeshi huwa na chemba zonazoshika risasi zaidi ya 100.

Aina za bunduki[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida neno lataja silaha za moto zenye kasiba ndefu zinazoshikwa mkononi.

  • Bunduki kubwa zaidi zinazosimama kwa magurudumu huitwa mzinga.
  • Bunduki ndogo yenye kasiba fupi ni bastola.
  • Bunduki kubwa kiasi inayofyatua risasi nyingi wakati moja ni bombomu (au: mzinga wa bombom; bunduki ya mtombo; bunduki ya rashasha).
  • Aina hii kama ndogo zaidi ni bunduki ya nusu mtombo.
  • Bunduki ya upepo inazotumia nguvu ya gesi yenye shindikizo bila mlipuko. Silaha ndogo ya aina hii shindikizo inapatikana kwa kukandamiza hewa katika chumba cha bunduki. Aina zenye nguvu zinatumia ramia isiyo na baruti bali na gesi iliyokandamizwa ndani yake. Faida yake ni hazina kelele kubwa.
  • Bunduki ya marisau hutumiwa kwa kuwinda wanyama ikifyatua risasi nyingi ndogondogo. Ni rahisi zaidi kushika shabaha lakini haipigi mbali.
  • Gobori ni bunduki ambako risasi na baruti zinaingizwa kupitia mdomo wake katika kasiba. Inapiga mara moja tu halafu ni lazima kuijaza upya. Aina hii ni silaha ya kihistoria lakini hupatikana pia kama silaha inayotengenezwa nyumbani.
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: