Kasiba
Kasiba ni sehemu ya silaha ya moto kama bunduki, bastola au mzinga. Kazi yake kwenye silaha ni kuipa risasi mweleko. Umbo lake ni kama bomba. Upande mmoja ni wazi huitwa mdomo ambako risasi inatoka. Upande mwingine ni mahali pa kuweka risasi.
Bunduki na mizinga ya kale zilijazwa risasi pamoja na baruti kupitia mdomo wa kasiba. Aina hii ya bunduki huitwa gobori. Hapa kwanza baruti halafu risasi husukumwa hadi mwisho wa kasiba inayofungwa isipokuwa kuna shimo dogo. Kwenye shimo hili moto huingizwa inayowasha baruti ndani ya kasiba; kulipuka au kuchomeka kwa ghafla kwa baruti inatokeza gesi inayosukuma risasi kufuatana na nafasi ya kasiba na kuipa nguvu na mwelekeo kwa mbio wake.
Kwa kawaida kasiba ndefu huongeza umakinifu wa kulenga unaopungua kama kasiba ni fupi kama kwenye bastola.
Tangu karne ya 19 kasiba imepewa mifuo ndani yake kwa mwendo wa sukurubu iliipa risasi mwendo wa kuzunguka na kuongeza ukamilifu wa kupiga shabaha.
Kwa kuongeza kasi ya kufyatulia kasubi zilitengezwa zikiwa na mfuniko wa nyuma unaoruhusu kuingiza risasi kutoka nyuma. Risasi na baruti ziliunganishwa katika ramia inayowashwa kwa pigo kali kwenye ganda la ramia.
Siku hizi silaha ndogo kama bunduki, bastola na bombomu zina chemba penye akiba ya ramia. Bastola huwa na ramia hadi 10, bunduki huwa na nafasi ya ramia hadi makumi na bombomu hushika fremu ya ramia mamia.