Nenda kwa yaliyomo

Zimbabwe African National Union

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka ZANU)

ZANU (Zimbabwe African National Union) ni chama cha kisiasi nchini Zimbabwe. ZANU imetawala tangu mwaka 1980.

Chama kilianzishwa mwaka 1983 kama farakano kutoka chama cha ZAPU na mchungaji Ndabaningi Sithole (1920-2000) pamoja na wakili Herbert Chitepo wasiopendezwa na mwelekeo mkali wa Joshua Nkomo kiongozi wa ZAPU na mweleko wake upane wa Umoja wa Kisovyeti.

ZANU kilikuwa chama kimoja kilichoendesha vita ya msituni dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza wa Rhodesia.

1975 kulitokea farakano baada ya kuuawa kwa Chitepo na azimio la Sithole la kutafuta usuluhisho bila mabavu wa vita ya ukombozi. Wakati ule ZANU iligeukia kuwa harakati wa Kishona ilhali Wandebele walisimama upande wa Sithole au kwa upande wa ZAPU. Katibu Mkuu Robert Mugabe alikuwa kiongozi mpya wa ZANU.

Baada ya amani ya Lancaster House ZANU chini ya Mugbe ilishinda uchaguzi kwa kura za Washona walio wengi nchini Zimbabwe.

Tangu mwaka ule ZANU imeendelea kama chama tawala wa Zimbabwe. 1988 kiliungana na ZAPU wa Joshua Nkomo na kutumia jina la ZANU-PF.