Bahari ya Eritrea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Bahari ya Eritrea (Kigiriki ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa) ni jina la kale la Bahari ya Shamu na Bahari Hindi. Neno "erythra" katika lugha ya Kigiriki inamaanisha rangi nyekundu ("thalassa" = bahari). Hivyo bahari ile iliitwa kwa jina kama "Bahari Nyekundu" (linganisha Kiing. "Red Sea"). Inasemekana ya kwamba jina hili limetokana na aina ya mwani unaoonyesha rangi hiyo wakati mwingine.

Inaonekana ya kwamba waandishi wa kale hawakutofautisha kati ya Bahari ya Shamu na Bahari Hindi. Merikebu za zamani zile zilitembea muda wote karibu na pwani kwa sababu dira haikulikana bado nje ya Uchina. Hivyo haikuwa rahisi kuvuka bahari moja kwa moja na kupata picha kamili ya umbo la bahari.

Nahodha wa merikebu hizi walitumia maandiko kama Periplus ya Bahari ya Eritrea wakipanga safari zao.