Nenda kwa yaliyomo

Mzunguko wa Bahari Nyekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majina, mahali na njia za biashara katika Periplus

Mzunguko wa Bahari Nyekundu (kwa Kiingereza: Periplous of the Erythrean Sea) ni kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mabaharia kilichoandikwa mnamo mwaka 70 BK.

"Periplous" ni neno la Kigiriki linalomaanisha tendo la kuzunguka bara kupitia bahari kwa merikebu; "Bahari ya Eritrea" ni jina la kale kwa ajili ya Bahari ya Shamu (hadi Bahari Hindi). Jina hilo lilitungwa na watu wa nchi za mashariki ya Bahari ya Kati na Misri waliotumia lugha ya Kigiriki miaka 2000 iliyopita.

Kitabu hicho kimeandikwa na mwenyeji wa Aleksandria / Misri uliokuwa mji mkubwa wakati ule na kitovu cha biashara ya kimataifa kati ya Dola la Roma, Afrika ya Mashariki na Bara Hindi.

Kitabu kinaeleza juu ya bandari kuanzia Misri hadi Afrika ya Mashariki kwa upande mmoja na hadi Bara Hindi kwa upande mwingine. Kinataja majina ya bandari, bidhaa zilizopelekwa huko na bidhaa zilizopatikana kila mahali. Pia kuna habari za kando juu ya watu, watawala na mila zao.

Maelezo ni mengi kuhusu pwani ya Eritrea na Somalia hadi Pembe ya Afrika; kuelekea kusini majina ya bandari ni machache; mwisho wa eneo lililojulikana ni mji wa Rhapta katika nchi za Azania, lakini hadi leo wataalamu hawajaelewana Rhapta na Azania zilikuwa wapi.

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzunguko wa Bahari Nyekundu kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.