Dogali
Mandhari
Dogali katika tambarare ya pwani la Eritrea takriban 30 km kutoka Massawa ni mahali pa mapigano yaliyotokea tarehe 24 Januari 1887 kati ya wanajeshi wa Italia na Ethiopia.
Kikosi cha Waitalia 587 kilielekea kaskazini kutoka Massawa kikashambuliwa kwenye kijiji cha Dogali na kushindwa na Ras Alula aliyekuwa mtemi chini ya Negus wa Ethiopia. Karibu Waitalia 500 waliuawa ni 80 wajeruhiwa pekee waliweza kurudi.
Kuna kumbukumbu ya mapigano kwenye obeliski huko Roma na makaburi ya Waitalia kwenye mahali penyewe ya kukumbuka waliokufa.