Dola la Mahdi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dola la Mahdi 1881-1898
Muhammad al-Mahdi

Dola la Mahdi (kwa Kiarabu المهدية, "mahdiyya") lilikuwa kipindi katika historia ya Sudan mwisho wa karne ya 19. Lilianzishwa na Muhammad Ahmad Al-Mahdi mwaka 1881 alipojitangaza kuwa mahdi kufuatana na imani ya kiislamu akaongoza uasi dhidi ya Misri iliyotawala Sudan ikisimamiwa yenyewe na Uingereza.

Mwanzo chini ya Muhammad Al-Mahdi[hariri | hariri chanzo]

Muhammad Ahmad Al-Mahdi alifaulu kukusanya wafuasi wengi na kushinda Wamisri. 26 Januari 1885 jeshi lake lilitwaa mji mkuu Khartum na kumwua gavana Gordon Pasha. Al-Mahdi alianzisha mji mkuu mpya ng'ambo ya mto Nile kwa kuunda Omdurman. Wamisri na Waingereza wakatoka nje ya Sudan.

Baada ya ushindi wake Al-Mahdi alikufa na homa ya matumbo.

Utawala wa khalifa Abdullahi[hariri | hariri chanzo]

Ugomvi ulitokea kati ya makamu zake hadi 1891 wakati Abdallahi ibn Muhammad, aliyewahi kuongoza jeshi la mahdi wakati wa mashambulio dhidi ya Khartum, alikubaliwa wa viongozi wa mahdiyya akajiita "khalifa".

Khalifa Abdullahi aliimarisha utawala wake wa kuwaua wapinzani bila neema kati yao wanafunzi na ndugu za mahdi mwenyewe. Akajenga jumba mjini Omdurman linalosimama hadi leo.

Khalifa Abdullahi alijaribu kutumia teknolojia mbalimbali. Akanunua meli za mvuke za mtoni alizoziona Waingereza walizitumia pia akajenga kiwanda cha kutengenezea bunduki. Akaanzisha nyaya za mawasilaino kwa simu. Lakini kwa ujumla vita na utawala wa mahdiyya zilikuwa ziliharubu uchumi iliyoendelea kuzorota.

Khalifa alifaulu kupanusha uatwala wake juu ya maeneo karibu yote ya Sudan ya leo lakini alishindwa kufikia jimbo la Ikweta ambako Emin Pasha aliendelea kutetea mabaki ya Sudani ya Kimisri.

Jeshi la Mahdiyya

Majaribio ya jihadi dhidi ya nchi jirani[hariri | hariri chanzo]

Itikadi ya kupanusha utawala wa mahdiyya kwa njia ya jihad ilimsababisha khalifa kushambulia nchi jirani ya Ethiopia iliyotawaliwa na kaisari wa kikristo. Mwaka 1887 akaongoza jeshi la askari 60,000 hadi Gondar. Waethiopia wakajibu kwa kushambulia Sudan 1889. Kifo cha Kaisari Yohane IV katika mapigano ya Metemma tar. 9 Machi 1889 ililazimisha Waethiopia kurudi kwao. Lakini jeshi ya mahdiyya lilipotea wanajeshi wengi pia likadhoofika.

Wakati huohuo jemadari wa khalifa Abd ar-Raħmān an-Nujumī alishambulia Misri lakini alishindwa kwenye mapiganoya Tushkah. Hii ilikuwa mara ya kwanza ya kwamba jeshi la mahdiyya lilishindwa.

Majaribio ya vita za jihadi dhidi ya Wabelgiji katika jimbo la Ikweta na dhidi ya Waitalia katika Eritrea yalishindikana pia.

Mapigano ya Omdurman 2 Septemba 1898

Waingereza kuteka Sudan[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1895 mkuu wa jeshi la pamoja la Misri na Uingereza jenerali Horatio Kitchener aliamua kulipiza kisasi kwa vita ya 1885 akaongoza jeshi kubwa dhidi ya Sudan. Kwa kutumia meli za mvuke kwenye mto Nile na kujenga reli akasongea mbele hadi Omdurman. Tar. 2 Septemba 1898 jeshi la mahdiyya lilishindwa kabisa katika mapigano ya masaa matano. Safari hii Waingereza waliandaliwa vizuri zaidi pia silaha mpya kama bunduki ya mtombo ziliwapa ushindi. Upande wa khalifa walikufa askari 11,000, upande wa Waingereza na Wamisri watu 400 pekee.

Khalifa mwenyewe alitoroka akajenga jeshi upya na kutawala kusini ya Sudan lakini akauawa 1899 katika mapigano ya Umm Diwaykarat.

Waingereza walitawala Sudan pamoja na Misri hadi 1956, Kitchener akawa gavana mkuu wa kwanza.