Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea
Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea ni madhehebu ya dini ya Ukristo iliyotawala makabila ya Eritrea kaskazini kwa karne kadhaa hadi sasa.
Wakristo hao wanaotaka kuzingatia imani sahihi ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Eritrea kama ulivyo kwa wenzao wa Ethiopia[1].
Kwa sasa lina waumini milioni 3.[2] wengi wao wakiishi nchini Eritrea,[3] lakini pia Ulaya na Amerika.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea linaendeleza ushirika na Kanisa la Misri tangu lilipoanzishwa na mtakatifu Frumensyo aliyetumwa na mtakatifu Atanasi, Patriarki wa Aleksandria ainjilishe ufalme wa Aksum katikati ya karne ya 4 BK.
Hata hivyo mwaka 1993 lilikubaliwa liwe na Patriarki wake mwenyeji na kujiongoza.
Kalenda
[hariri | hariri chanzo]Kufuatana na mapokeo ya huko Misri, Epifania na Pasaka ni sikukuu muhimu sana, na husherehekewa kwa kufanya mambo kama vile kufunga kula na kucheza.
Pia kuna siku kadhaa katika mwaka ambapo ni mboga za majani pekee na samaki ndio huruhisiwa kuliwa.
Desturi
[hariri | hariri chanzo]Ndoa huweza kuanzishwa au kupangwa wakati mwanamume ana umri wa miaka kumi na..., au ishirini na... Kiutamaduni, wasichana wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18, lakini katika karne ya 20, mambo yamebadilika, hivyo sasa umri mdogo kuliko wote wa kuolewa ni miaka 18, na suala hili linasimamiwa na serikali. Ndoa za kiserikali ni nyingi japo pia, wapo watu wanaofunga ndoa katika makani mbalimbali. Na baada ya kufunga ndoa kanisani, suala la talaka halipo na haliwezekani. Kila familia hufanya sherehe ya ndoa baada ya harusi.
Tangu kuzaliwa, padri hutembelea familia kwa ajili ya kumbariki mtoto, na pia kutahiri mtoto kama ni wa kiume. Mama wa mtoto, hutakiwa kukaa ndani kwa siku 40 baada ya kujifungua kama mtoto ni wa kiume na kukaa ndani kwa siku 80 kwa mtoto ni wa kike kabla ya kwenda kanisani kwa ajili ya ubatizo.
Sanaa
[hariri | hariri chanzo]Sanaa ya nchini Eritrea kwa ujumla imeegamia katika masuala ya dini na michoro ya dini.
Mmoja kati ya michoro mizuri zaidi ya vitu au watu wenye macho makubwa na mara nyingi huwa ni watu wanaohusiana na Biblia.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ FDRE States: Basic Information - Amhara Archived 10 Machi 2007 at the Wayback Machine., Population (accessed 26 Machi 2006)
- ↑ "Ethiopia: Orthodox Head Urges Churches to Work for Better World". Iliwekwa mnamo 2006-09-13.
- ↑ Berhanu Abegaz, "Ethiopia: A Model Nation of Minorities" (accessed 6 April 2006)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Eritrean Orthodox Tewahedo Church
- Article on Eritrean Orthodox Church by Ronald Roberson on the CNEWA website.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |