Ufalme wa Aksum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mji wa Aksum na Uarabuni ya Kusini mwishoni mwa karne ya tatu BK.

Ufalme wa Aksum (pia: Axum) (Ge'ez: አክሱም), ulikuwa milki muhimu katika karne za kwanza baada ya Kristo. Uliunganisha sehemu ya za nchi za leo Ethiopia ya kaskazini, Eritrea, Sudan na Yemen. Mji mkuu Aksum liko katika Ethiopia ya leo. Milki hii ilianzishwa mnamo karne ya 1 KK ikaishia wakati wa karne ya 7 BK.

Hakuna uhakika juu vyanzo vya Aksum. Inatajwa kama milki muhimu katika Periplus ya Bahari ya Eritrea iliyoandikwa mnamo mwaka 70 BK. Wakati ule ilitawala tayari bandari muhimu ya Adulis kwenye pwani la Bahari ya Shamu. Kutokana bandri hii muhimu Aksum ilikuwa na nafasi ya kutawala sehemu ya biashara ya kimataifa kati ya Dola la Roma na Uhindi. Meli za nyakati zile zilikuwa jahazi zilizofuata pwani zikategemea mabandari njiani na jahazi zote zilisafiri kati ya Misri ya Kiroma hadi Uhindi zilitegemea kituo cha Adulis.

Tangu kufifia kwa milki ya Kushi katika Sudan ya leo Aksum ilipanuka upande ule. Ilivuka pia bahari na kupanusha eneo lake katika Uarabuni ya kusini sehemu za Yemen ya leo.

Chini ya Mfalme Ezana Aksumu ilikuwa ya kwanza kubadili dini na kuwa wakristu na kupenwa jina la Mani, ambaye ni moja kati ya mitume wanne wanne waliokuwa na ushawishi mkubwa.[1][2]

Kumbukumbu za Kihistoria[hariri | hariri chanzo]

Aksumu imetajwa katika karne ya kwanza kama Periplus of the Erythraean Sea kama sehemu muhimi ya masoko ya meno ya ndovu, yaliyokuwa yakitumwa katika sehemu mbalimbali duniani, chini ya Mfalme katika karne ya kwanza Zoskales ambaye pamoja na kuongoza Aksum, pia aliweza kuongoz pwani mbili za Red Sea na (Assab) iliyopo nchini Eritrea pia mfalme huyu anafahamika kuwa alikua na ujuzi fulani wa maandishi wa kigiriki .[3]

Himaya[hariri | hariri chanzo]

Katika kipindi cha kupata mafanikia zaidi, Himata ya Aksum, ilifanikiwa kujitanua hadi kufikia katika nchi inayojulikana sasa kama Eritrea Kaskazini mwa Ethiopia, Yemen, Kusini mwa Saudi Arabia na kaskazini mwa Sudan. Mjii mkuu wa Aksun ulijulikana kama Axum kwa sasa ukiwa kaskazini mwa Ethiopia Katika karne ya 3, Aksum ilianza kuingilia masuala ya ndani ya nchi kama vile Arabia ya Kusini, na wakati kwa wakati waliweza kuongoza Magharibi mwa mji wa Tihama. Pia iliweza kuongoza baadhi ya maeneo katika Penisula ya Arabia na Bahari nyekundu na kuwafanya walipe fedha kwa utawala wa Aksum.[4] . Katika mwishoni mwaka karne ya tatu, Aksum ilianza kutengeneza sarafu yake yenyewe na kuipa jina la Mani aliyekuwa moja katika ya mitume wanne wa kipindi hicho

Kuanguka[hariri | hariri chanzo]

Hatimaye utawala wa kiislam ulifanikiwa kuchukua Red Sea, na maeneo mengi ya Mto Nile na hivyo kuulazimisha utawala wa Axum, kujitenga katika shughuliza za kiuchumi .[4] Northwest of Axum (in modern day Sudan), Christian states of Maqurra and Alwa lasted till the 13th century before becoming Islamic.[4] Axum, isolated, nonetheless still remained Christian.[4] Katika sehemu ya pili ya golden age, hii ikiwa ni katika karne ya 6, utawala huu ulianza kuanguka na hatimaye kupotea kabisa uwezo wake wa kuzalisha sarafu. Wakati wa kipindi hiki, wakazi wa maeneo ya Aksum, walilazimika kuingia ndani zaidi katika himaya hiyo kwa sababu za kiusalama. Historia za kijadi zinaandika kuwa, Malkia wa Kiyahidi, aliyejulikana kama (Judith) au "Gudith" aliiweza kuuangusha utawala wa Aksum, akachoma makanisa yaliyokuwapo hapa pamoja na kumbukumbu za kiimaandishi . Lakini japokuwa tayari kuna ushahidi wa makanisa yaliyochomwa moto, bado suala la kuwapob kwa Malkia huyu katika eneo la Aksum, limeenedelea kujadilia siku hadi siku na waandishi mbalimbali. Sababu nyingine ya kuanguka kwa utawala wa Aksum ni pamoja na Mabadiliko ya tabia nchi na kutengwa kimasoko. Matumizi ya ardhi kupita kiasi pia yalichangia ardhi katika maeneo hayo kushindwa kuzalisha mazao yenye rutuba na hivyo kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula. Pia hali hii ilisababisha na kubadilika kwa kutiririka kwa maji ya mto Nile na ukame.

Mahusiano ya kigeni, masoko na uchumi[hariri | hariri chanzo]

Aksum ilikuwa ni moja wa wachangiaji wakubwa katika masoko ya kimataifa katika karne ya kwanza AD.
Umuhimu kwa maeneo mbalimbali ya uzalishaji wa hariri na viungo, pamoja na misafara yake.

Mazao makubwa yaliyokuwa yakitumwa nje ya Axum, yalikuwa zaidi mazao ya kilimo, kama vile shahiri. Watu wa Aksum hali kadhalika waliweza kufuga kondoo, ng'ombe na ngamia. Wanyama wakali walikuwa waliwindwa na kutoa vitu kama meno ya ndovu. waliweza kufanya kazi na na wafanyabiashara kutoka Misri na Persian. Pia walikuwa na utajiri wa dhahabu na madini ya chuma, na chumvi

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Vidokezo[hariri | hariri chanzo]

 1. Stuart Munro-Hay, Aksum: An African Civilization of Late Antiquity. Edinburgh: University Press, 1991, p. 57.
 2. Paul B. Henze, Layers of Time: A History of Ethiopia, 2005.
 3. Periplus of the Erythreaean Sea, chs. 4, 5
 4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Civilizations of Africa: Axum

Bibliografia[hariri | hariri chanzo]

 • Francis Anfray. Les anciens ethiopiens. Paris: Armand Colin, 1991.
 • Carlo Conti Rossini. Storia d'Etiopia. Bergamo: Istituto Italiano d'Arti Grafiche, 1928.
 • Stuart Munro-Hay. Aksum: A Civilization of Late Antiquity. Edinburgh: University Press. 1991. ISBN 0-7486-0106-6
 • Yuri M. Kobishchanov. Axum (Joseph W. Michels, editor; Lorraine T. Kapitanoff, translator). University Park, Pennsylvania: Penn State University Press, 1979. ISBN 0-271-00531-9
 • Karl W. Butzer. Rise and Fall of Axum, Ethiopia: A Geo-Archaeological Interpretation. American Antiquity, Vol. 46, No. 3. (Jul., 1981), pp. 471–495.
 • Joseph W. Michels. Changing settlement patterns in the Aksum-Yeha region of Ethiopia: 700 BC - AD 850 (BAR International Series 1448) Oxford: Archaeopress, 2005.
 • Mukhtār, Muḥammad Jamāl al-Dīn. 1981. Ancient civilizations of Africa. General history of Africa, 2. London: Heinemann Educational Books.ISBN 978-0-435-94805-4
 • David W. Phillipson. Ancient Ethiopia. Aksum: Its antecedents and successors. London: The British Museum, 1998.
 • David W. Phillipson. Archaeology at Aksum, Ethiopia, 1993-97. London: British Institute in Eastern Africa, 2000.
 • Williams, Stephen. "Ethiopia: Africa's Holy Land". New African, Vol. 458. ( Jan., 2007), pp 94–97.
 • Belai Giday. Ethiopian Civilization. Addis Ababa, 1992

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]