Historia ya China

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo yaliyotawaliwa na nasaba mbalimbali katika urefu wote wa historia ya China.

Historia ya China inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Watu wa China lakini hasa maeneo yote yanayopakanwa na Nyanda za Juu za Tibet upande wa magharibi, Jangwa la Gobi upande wa kaskazini, Myanmar (Burma), Laos na Vietnam upande wa kusini- magharibi na bahari upande wa mashariki. [1]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Jamii za kwanza zilizoendelea kuwa sehemu za utamaduni wa Kichina zilikalia bonde la Mto Huang He (Mto Njano). Kutoka hapa zilienea polepole zikiathiri makabila mengine. Wakati wa Nasaba ya Han (206 KK – 220 KK) , maeneo mengi ya china ya kihistoria yaliathiriwa tayari na utaaduni ulioanzishwa kwenye kaskazini. Kote hapa ilienea polepole lugha ya kimaandishi ya pamoja, imani kwa nguvu ya mbingu na mizimu na mtazamo wa pamoja kuhusu umuhmu wa matendo na sadaka maalumu zinazolenga kujenga upatanifu mzuri baina ya mbingu, mazingira asilia na binadamu.

Historia ya China hugawanyika katika vipindi vya nasaba za kifalme mbalimbali. Vipindi muhimu zaidi ni kama ifuatavyo:

Nasaba kabla ya maungano ya China[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuunganiswa kwa China kulikuwa na madola mbalimbali. Kati ya madola hayo kuna hasa nasaba tatu zilizoacha ushahidi wa kihistoria:

Katika kipindi hicho yalitokea mabadiliko kutoka teknolojia ya mawe hadi bronzi na baadaye chuma. Misingi ya falsafa na dini ya Utao na pia Ukonfusio iliwekwa wakati wa Zhou.

Nasaba tangu kuunganishwa kwa China[hariri | hariri chanzo]

Utawala wa kifalme uliendelea hadi mapinduzi ya China ya 1911.

Baada ya kipindi cha vurugu, jamhuri ya China ilitawaliwa na chama cha Kuomintang chini ya rais Chiang Kai-shek.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia sehemu kubwa za nchi ilitwaliwa na Japani. Wakati huo Chama cha Kikomunisti cha China kiliandaa jeshi kikapambana na serikali ya Kuomintang na Japani pia.

Baada ya mwisho wa vita kuu Wakomunisti waliendelea kupingana na serikali na mwaka 1949 Kuomintang ilishindwa. Wakomunisti chini ya Mao Zedong walianza kutawala China Bara kama Jamhuri ya Watu wa China na Kuomintang walikimbilia kisiwa cha Taiwan walipoendelea kutawala kama "Jamhuri ya China".

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya China kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Chinese painting, tovuti ya Britannica, iliangaliwa Mei 2023