Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Kuwait

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Kuwait inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Kuwait.

Historia ya Kuwait ilianza kama utemi mdogo chini ya familia ya Al-Sabah iliyokuwa chini ya Sultani wa Uturuki aliyetawala nchi jirani ya Irak hadi vita vikuu vya kwanza vya dunia.

Tangu kuingia kwa Waingereza katika nchi za Ghuba ya Uajemi, mwaka 1899 watawala wa Kuwait walijiweka chini ya ulinzi wa Uingereza kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki.

Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya Waosmani na baadaye dhidi ya Saudia.

Baada ya kuporomoka kwa dola la Uturuki Kuwait iliendelea kama nchi lindwa chini ya Uingereza hadi kupata uhuru wake tarehe 19 Juni 1961.

Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai ya Irak ya kuwa tangu zamani Kuwait ni mkoa wake uliotengwa na wakoloni tu.

Tarehe 2 Agosti 1990 dikteta wa Irak Saddam Hussein alivamia Kuwait na kuiteka. Katika vita vya pili vya Ghuba Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambulia jeshi la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali ya Emir al Sabah.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Kuwait kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.