Historia ya Singapore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Singapore inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Singapura.

Kisiwa hicho kiliwahi kuwa na makazi mbalimbali katika historia.

Mji wa kisasa ulianzishwa mwaka 1819 na Waingereza kama kituo cha biashara ikawa bandari muhimu ya eneo.

Uingereza uliipa uhuru kama sehemu ya shirikisho la Malaysia. Lakini matatizo ya kuelewana yalionekana haraka kati ya wanasiasa Wamalay wa bara na wenzao Wachina wa kisiwani.

Mwishowe Singapuri ikafukuzwa katika shirikisho ikawa nchi ya kujitegemea tarehe 9 Agosti 1965. Mwanasiasa Lee Kuan Yew alikuwa waziri mkuu wa kwanza akaendelea na cheo hicho hadi mwaka 1990 akaongoza Singapuri kuwa kati ya mataifa tajiri ya Asia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Singapore kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.