Historia ya Bahrain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya mwaka 1745 iliyochorwa na Bellin ikionyesha Bahrain.

Historia ya Bahrain inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Bahrain.

Bahrain ndiyo makao ya ustaarabu wa Dilmun. Ilipata umaarufu tangu zamani kwa kuvua lulu bora kuliko zote duniani hadi karne ya 19.

Bahrain ilikuwa kati ya maeneo ya kwanza kuongokea Uislamu, mwaka 628 BK.

Baada ya kipindi cha utawala wa Waarabu, Bahrain ilitekwa na Wareno mwaka 1521 hadi 1602 walipofukuzwa na Shah Abbas I wa nasaba ya Safavid chini ya Dola la Uajemi.

Mwaka 1783, ukoo wa Bani Utbah uliteka Bahrain kutoka kwa Nasr Al-Madhkur na tangu hapo nchi imetawaliwa na ukoo wa Al Khalifa, Ahmed al Fateh akiwa hakimu wa kwanza wa Bahrain.

Tangu mwaka 1820 Visiwa hivyo pamoja na Qatar na Falme za Kiarabu vilikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Tangu mwaka 1820 hao walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Bahrain kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.