Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Myanmar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Myanmar inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya muungano wa Myanmar.

Tangu karne ya 9 BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa Pagan.

Katika karne ya 19 Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (leo Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa vita vitatu kati ya miaka 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake.

Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu mwaka 1885.

Mwaka 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni la pekee.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Japani ilitwaa karibu nchi yote.

Baada ya vita hivyo Burma ikapata uhuru wake tarehe 4 Januari 1948.

Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa na jeshi mwaka 1962.

Mtawala mpya hadi mwaka 1988 alikuwa jenerali Ne Win aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa vikali mara kadhaa.

Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu.

Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa, Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi.

Uchaguzi huru wa mwaka 1989 ulileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhi madaraka.

Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi hadi mwaka 2011. Upinzani haukuruhusiwa.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Myanmar kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.