Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Nepal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Nepal inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya kidemokrasia ya shirikisho la Nepal.

Vyombo vya watu waliokuwa wakiishi katika zama za mawe zilipatikana katika bonde la Kathmandu kuonyesha kwamba kumekuwa na watu waliokuwa wakiishi katika eneo hili la Himalaya kwa muda wa zaidi ya miaka elfu kumi na moja. Maandishi makongwe yanaonyesha kwamba Nepal ilikuwepo hata miaka 30 kabla ya ujio wa Yesu Kristo.

Viongozi wa kwanza nchini Nepal walikuwa wanaKirati. Historia ya Nepal yaonyesha kwamba kulikuwa na himaya 30 hivi za wanaKirati walioongoza nchi hii.

Kisiasa Nepal iko katika kipindi cha mageuzi. Hadi mwaka 2006 mfalme alitawala peke yake baada ya kuvunja bunge. Mwaka huo alilazimishwa kurudisha bunge, nalo lilitangaza ya kwamba mfalme hana mamlaka tena likamteua Mkuu wa nchi kwa muda. Tena kwamba bunge jipya litakalochaguliwa mnamo Juni 2007 litaamua juu ya katiba mpya.

Tarehe 28 Mei 2008 wananchi waliamua kumaliza ufalme Nepal ikatangazwa kuwa jamhuri inayofuata demokrasia na kuwa na muundo wa shirikisho.

Katiba mpya ilipitishwa mwaka 2015.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Nepal kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.