Nenda kwa yaliyomo

Kathmandu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Kathmandu
Nchi Nepal
Mahekalu kwenye uwanda wa Durbar mjini Patan

Kathmandu (kwa Kinepali: काठमाडौं, काठमान्डु) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Nepal wenye wakazi milioni 1.5. Iko katika bonde la Kathmandu kando ya mto Bagmati kwenye milima ya Himalaya kwa kimo cha mita 1,300. Miji ya Patan na Bhaktapur iko karibu. Mahali pake ni 27°43′N 85°22′E.

Mji una mahekalu mengi mazuri ya Uhindu na Ubuddha pamoja na nyumba za kihistoria. Bonde lote la Kathmandu liliingizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kathmandu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.