Historia ya Yordani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Yordani inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Yordani.

Nchi ya sasa ilianzishwa kwa jina la "Transjordan" (ng'ambo ya mto Yordani) kama sehemu ya eneo la Palestina lililotawaliwa na Uingereza kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa baada ya mwaka 1918.

Waingereza waliamua kutenganisha eneo hilo na Palestina upande wa magharibi wa mto Yordani na kuliweka tangu mwaka 1921 chini ya mamlaka ya Abdullah bin al-Husayn wa familia ya Wahashemi aliyekuwa mtoto wa Sharif wa Makka wa mwisho kabla ya mji huu kutwaliwa na Wasaudi.

Kwa hatua hii Uingereza ililenga kuimarisha uhusiano wake na makabila ya Waarabu wa jangwa. Abdullahi alitawala awali kwa cheo cha emir baadaye kama mfalme wa "Transjordan".

Jeshi lake lilishiriki katika vita vya mgawanyo wa Palestina na Israeli miaka 1948-1949 na kushika sehemu ya Palestina isiyotawaliwa na Israeli.

Baada ya vita vya siku sita ya mwaka 1967 maeneo yote upande wa magharibi wa mto Yordani yalipotawaliwa na mfalme Hussein II, mwandamizi wa Abdallah tangu mwaka 1952.

Mwishowe aliacha madai yote ya utawala juu ya sehemu hizo.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Yordani kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.