Historia ya Afghanistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Historia ya Afghanistan inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Afghanistan.

Afghanistan kama nchi ya pekee ilianza kutokea katika karne ya 19. Kabla ya hapo nchi yote au sehemu mbalimbali zilikuwa sehemu ya milki jirani hata kama sehemu za eneo la Afghanistan zilijitegemea chini ya watawala wadogo. Kwa vipindi virefu vya historia Afghanistan ilikuwa sehemu ya milki za Uajemi (Iran).

Tangu miaka ya 1980 Afghanistan imekabiliwa na vita; mwaka 1979 Umoja wa Kisovyeti ulivamia nchi lakini ukapaswa kujiondoa tena mwaka 1989.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilifuata kati ya vikundi vya wapinzani ambako nchi jirani ya Pakistan ilikuwa na athira kubwa kwa kutuma silaha na pesa.

Baada ya kipindi kifupi cha serikali ya kitaifa, kundi la Kiislamu la Taliban lilifaulu kuteka Kabul kwa msaada kutoka Saudia na Pakistan mwaka 1997.

Serikali ya Taliban ilikwisha kwa sababu walimruhusu Osama bin Laden pamoja na kundi lake la Al-Qaide kuwa na kimbilio nchini. Baada ya Shambulio la 11 Septemba 2001 Marekani ililipa kisasi kwa kushambulia Afghanistan.

Hali ya vita imeendelea ndani ya Afghanistan katika vita ya Marekani na NATO 2001-2014. Tangu Disemba 2014 nchi za NATO zilitangaza ya kwamba wamemaliza kuhudhuria katika mapigano na kuondoa sehemu kubwa ya wanajeshi kutoka Afghanistan. Vikosi vya NATO vimebakizwa shabaha ya kusaidia jeshi la kitaifa.

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Afghanistan kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.