Historia ya Qatar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Qatar inahusu eneo ambalo leo linaunda nchi ya Qatar.

Maeneo ya Qatar, pamoja na Falme za Kiarabu na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao.

Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.

Miaka ya mwisho Qatar imejihusisha na siasa ya Mashariki ya Kati kwa kuwapa silaha Waislamu wenye itikadi kali kama vile huko Palestina, Syria na Iraq, na hata DAISH.

Kwa sababu hiyo imetengwa na nchi jirani, hasa Saudia.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Qatar kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.