Nenda kwa yaliyomo

Chifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chifu (kutoka Kiingereza: "chief"; majina ya kienyeji ni mengi tofautitofauti) ni kiongozi wa jadi katika kabila fulani.

Uongozi huo ulijitokeza mwishoni mwa zama za mawe na kutawala zama za chuma, mara nyingi ukisaidiwa na halmashauri ya wazee.

Wakati wa ukoloni, uongozi huo uliweza kukubalika, mradi uwe chini ya himaya ya wakoloni.

Hata baada ya uhuru, machifu wanaweza kuwa na madaraka fulani, k.mf. nchini Uganda.