Historia ya Bangladesh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Bangladesh inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Bangladesh.

Bangladesh ni sehemu ya mashariki ya Bengali ya kihistoria ambayo ilikuwa ndani ya Uhindi wa Kiingereza hadi 1947.

Mwaka 1857 Wahindi walipinga utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa na serikali yenyewe ya Uingereza kama koloni (1858).

Mwisho wa karne ya 19 harakati za Wahindi kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru.

Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu".

Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.

Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi. Bengali yenyewe iligawanyika kwa sababu wakazi wengi wa mashariki walikuwa Waislamu, tofauti na Wabengali wengine waliokuwa Wahindu.

Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.

Wakati ule Bengali ya mashariki ilikuwa nchi moja pamoja na Pakistan ya leo, bila kujali umbali mkubwa kati ya pande hizo mbili zilizounganishwa na dini.

Iliitwa "Pakistan ya Mashariki" mpaka mwaka 1971 ilipojitenga na Pakistan kwa msaada wa India katika Vita vya Uhuru vya Bangla Desh.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Bangladesh kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.