Historia ya Armenia
Historia ya Armenia inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Armenia.
Armenia ni kati ya mataifa ya kale kabisa duniani, ingawa eneo lake limebadilika sana na lile la sasa ni sehemu ndogo tu ya maeneo yaliyokuwa ya Armenia katika karne na milenia zilizopita.
Armenia ilikuwa nchi ya kwanza kupokea Ukristo kama dini rasmi ya kitaifa mnamo mwaka 301. Hadi leo zaidi ya 93% za Waarmenia ni Wakristo wa Kanisa la kitaifa ambalo ni mojawapo kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki.
Jambo hilo lilichangia sana mateso yaliyowapata kutoka kwa majirani ambao wengi wao ni Waislamu, hasa Waturuki waliotawala kwa karne nyingi maeneo makubwa ya Dola la Osmani hadi Afrika na Ulaya.
Kilele chake kilikuwa maangamizi ya Waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo waliuawa zaidi ya milioni moja.
Armenia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti tangu 1920 hadi ilipopata uhuru wake tena mwaka 1991.
Kuna fitina na nchi jirani ya Azerbaijan kuhusu eneo la Nagorno-Karabakh linalokaliwa na Waarmenia lakini ni sehemu ya Azerbaijan kisiasa. Mipaka hii ni urithi wa zamani za Umoja wa Kisovyeti. Palikuwa na vita kati ya nchi hizo mbili. Hali halisi Armenia inatawala eneo hili ingawa Nagorno Karabakh ilijitangaza kuwa jamhuri ya kujitegemea isiyokubaliwa na umma wa kimataifa.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Armenia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |