Historia ya Luxemburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Luxemburg inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Ufalme mdogo wa Luxemburg.

Luxemburg kama nchi ndogo ilikuwa mara nyingi chini ya athira ya majirani wakubwa waliotawala juu yake kwa vipindi mbalimbali.

Kwa vipindi vingi vya historia yake Luxemburg ilikuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma.

Katika karne ya 14 watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani.

Baada ya vita vya Napoleon Bonaparte, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye Mkutano wa Vienna (1815) ya kurudisha Luxemburg kama nchi ya pekee itakayotawaliwa na Mtemi Mkubwa. Mfalme wa Uholanzi alikuwa mtemi wa Luxemburg na nchi yenyewe ilijiunga katika Shirikisho la Ujerumani.

Baada ya mwisho wa Shirikisho la Ujerumani (1866) Luxemburg haikujiunga (1870) na Dola jipya la Ujerumani.

Badiliko la familia ya kifalme katika Uholanzi lilisababisha uchaguzi wa mtemi wa pekee.

Ikiwa na wakazi 550,000 kwenye eneo la km² 2,586 pekee ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya, tena ilikuwa kati ya nchi sita zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya mwaka 1957.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Luxemburg kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.