Historia ya Eire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Eire inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Eire.

Kwa karne kadhaa Eire ilitawaliwa na Uingereza.

Sheria ya mwaka 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Muungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).

Baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.

Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee.

Baada ya uhuru wa sehemu kubwa ya kisiwa hicho, ile ya kaskazini-mashariki imebaki kama sehemu ya Ufalme wa Muungano.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Eire kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.