Historia ya Hispania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Historia inahusu eneo la Ulaya ambalo wakazi wake leo wanaunda Ufalme ya Hispania.

Historia ya awali[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Hispania walikuwa Wakelti.

Katika karne za 1 KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.

Waroma[hariri | hariri chanzo]

Waroma wa Kale walivamia na kutawala Hispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Hispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.

Katika karne ya 5 makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Hispania. Kati yao Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Hispania.

Waarabu[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Hispania hadi karibu milima ya Pirenei, lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao.

Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.

Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini kwa nchi.

Hatimaye mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada, mji wa mwisho wa Waarabu, alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.

Makoloni ya Amerika[hariri | hariri chanzo]

Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Hispania walimkubalia nahodha Kristoforo Kolumbus kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.

Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Hispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.

Katika miaka mia tatu iliyofuata Hispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.

Vita vya Marekani dhidi ya Hispania[hariri | hariri chanzo]

Vita hivyo vilitokea mwaka 1898. Vilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico vilivyokuwa koloni la Hispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Hispania huko Manila (Ufilipino) liliposalimu amri.

Vita hivyo vilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hivyo Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.

Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Hispania.

Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Hispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.

Hispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia.

Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Hispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.

Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Hispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Hispania kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.