Historia ya Polandi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya Polandi chini ya Mieszko I, mwanzilishi wa taifa (960–992).
Shirikisho la Warsaw katika kilele cha uenezi wake (1635).

Historia ya Polandi inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Polandi.

Waslavi walienea kati nchi katika nusu ya pili ya karne ya 5 BK.

Ukristo wa Kikatoliki kupokewa na mfalme Mieszko I (960-992) na Wapolandi kwa jumla (966) hutazamiwa kama chanzo cha taifa lao la pekee katika jamii ya Waslavi.

Nchi ilistawi na kuenea hasa chini ya ukoo wa Jageloni (13861572).

Kuanzia mwaka 1764 nchi ilianza kurudi nyuma na zile za jirani ziligawana kwa awamu tatu (1772, 1793, 1795) eneo lake lote.

Wapolandi walijaribu mara kadha kujikomboa, lakini walipata uhuru kwa muda tu (1807-1815 na 1918-1939).

Baada ya vita vikuu vya pili, Polandi ikawa chini ya utawala wa Kikomunisti hadi ilipofaulu kujikomboa (1989).

Poland imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Polandi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.