Historia ya Serbia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
ramani ya Serbia
bendera ya Serbia

Historia ya Serbia inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Serbia.

Waslavi walihamia Balkani baada ya karne ya 6.

Kati yao, Waserbia waliunda falme mbalimbali mwanzoni mwa Karne za Kati.

Mwaka 1217 Ufalme wa Serbia ulitambuliwa na Roma na Bizanti na mwaka 1346 ulifikia kilele cha ustawi wake kama Dola la Serbia.

tamaduni ya Lepenski Vir , 7000 BC
tamaduni ya Vinča , 4000–4500 BC

Hali hiyo haikudumu muda mrefu, tena katikati ya karne ya 16 eneo lote la Serbia ya leo lilitekwa na Waosmani, ingawa pengine sehemu yake ilitawaliwa na Dola la Wahabsburg.

Mwanzoni mwa karne ya 19, mapinduzi ya Serbia ilileta ufalme wa kikatiba wa kwanza katika Balkani.

Ufalme huo ulizidi kuenea na baada ya vita vikuu vya kwanza vilivyosababisha vifo vingi vya raia zake, Serbia iliungana na makabila kuanzisha Yugoslavia iliyodumu hadi miaka ya 1990 iliposambaratika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 2006 hata Montenegro ilitengana na Serbia, ila kwa amani.

Mwaka 2008 bunge la jimbo la Kosovo lilijitangazia uhuru.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Serbia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.