Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Ujerumani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Ujerumani inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.

Makabila mbalimbali ya Wagermanik yamekuwa yakiishi kaskazini mwa Ujerumani wa leo tangu zamani za Roma ya Kale. Eneo lililoitwa kwa Kilatini "Germania" linajulikana tangu mwaka 100 BK.

Kuanzia mwaka 400 hivi, wakati wa Dola la Roma kudhoofika, makabila hayo yalisambaa hasa kwenda kusini.

Mnamo mwaka 800 Karolo Mkuu, mtawala wa Wafaranki, aliunganisha maeneo ya Ujerumani na Ufaransa ya leo akaendelea kutwaa Italia ya Kaskazini na ya Kati hadi Roma. Mwaka 800 Papa alimpa cheo cha "Kaisari wa Roma". Baada ya kifo chake himaya iligawanyika, na upande wa mashariki hatimaye viongozi wa makabila walikutana mwaka 919 wakamchagua mfalme kati yao anayehesabiwa kuwa mfalme wa kwanza wa Wajerumani.

Kuanzia karne ya 10 wafalme wa Ujerumani walikuwa pia wadhamini wa Papa wa Roma aliyeendelea kuwapa cheo cha "Kaisari". Hivyo himaya yao iliitwa Dola Takatifu la Kiroma.[1]

Katika karne ya 16 maeneo ya Ujerumani kaskazini yakawa kiini cha Matengenezo ya Kiprotestanti katika Ukristo.

Baada ya Dola Takatifu kusambaratika, Shirikisho la Ujerumani ulianzishwa mwaka 1815.

Mwaka 1871, Ujerumani ukawa taifa-dola chini ya Prussia.

Kisha kushindwa katika vita vikuu vya kwanza, hilo Dola la Ujerumani lilikoma na kuiachia nafasi Jamhuri ya Weimar.

Adolf Hitler aliposhika uongozi wa nchi mwaka 1933 aligeuza nchi kuwa wa kidikteta na kuingiza dunia katika vita vikuu vya pili ambapo hasa Wayahudi waliangamizwa kwa mamilioni katika makambi maalumu.

Baada ya kushindwa tena vitani, nchi iligawanyika pande mbili, magharibi chini ya Marekani, Uingereza na Ufaransa, na mashariki chini ya Muungano wa Kisovyeti.

Ukomunisti ulipopinduliwa mwaka 1989, tarehe 3 Oktoba 1990 Ujerumani mashariki ulijiunga na shirikisho la Ujerumani magharibi ambao ulikuwa tayari kati ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Ulaya wa leo.[2]

Katika karne ya 21 Ujerumani ni nchi ya kidemokrasia yenye maendeleo makubwa hasa upande wa uchumi.

Kulingana na hatua za historia yake ndefu, inafaa kusoma kurasa zifuatazo:

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Ujerumani kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. The Latin name Sacrum Imperium (Holy Empire) is documented as far back as 1157. The Latin name Sacrum Romanum Imperium (Holy Roman Empire) was first documented in 1254. The full name "Holy Roman Empire of the German Nation" (Heiliges Römisches Reich Deutscher Nation, short HRR) dates back to the 15th century.
    Zippelius, Reinhold (2006) [1994]. Kleine deutsche Verfassungsgeschichte: vom frühen Mittelalter bis zur Gegenwart [Brief German Constitutional History: from the Early Middle Ages to the Present] (kwa German) (tol. la 7th). Beck. uk. 25. ISBN 978-3-406-47638-9.{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  2. Demshuk, Andrew (30 Aprili 2012). The Lost German East. ISBN 9781107020733. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Desemba 2016. {{cite book}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)