Jamhuri ya Weimar
Jamhuri ya Weimar (Kijerumani: Weimarer Republik) ilikuwa kipindi cha historia ya Ujerumani kuanzia 1919 hadi 1933.
Asili yake
[hariri | hariri chanzo]Mapinduzi ya Kijerumani ya Novemba 1918 yalimaliza utawala wa Kaisari katika Dola la Ujerumani baada ya kushindwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Ujerumani ikawa jamhuri, lakini bado iliitwa "Deutsches Reich" (Dola la Ujerumani). Kipindi kilichofuata kilileta tangazo la jamhuri na kuundwa kwa katiba mpya kwa Dola la Ujerumani kwenye bunge la katiba lililokutana katika mji wa Weimar. Kutokana na katiba iliyokubaliwa mjini Weimar kipindi chote kilichofuata huitwa "Jamhuri ya Weimar" na wataalamu wa historia. Jamhuri ya Weimar ilikwisha 1933 wakati Adolf Hitler alichaguliwa kama chansela wa Ujerumani na kuanzisha udikteta wa Dola la Tatu.
Kuanzishwa kwa jamhuri
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 9 Novemba 1918, Jamhuri ikatangazwa na Bw. Philipp Scheidemann katika jengo la Reichstag la mjini Berlin na masaa mawili baadaye jamhuri ya kisoshalisti ikawa ikatangazwa kwenye kona ya jumba la kifalme la Berlin na taarifa zilikuwa zikitolewa na Bw. Karl Liebknecht.
Baada ya tukio hilo, Kaisari Wilhelm II wa Ujerumani, akakimbilia nchini Uholanzi kiuhamisho na Jamhuri ikatangazwa rasmi kabla ya kwisha kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Matatizo ya jamhuri
[hariri | hariri chanzo]Jamhuri ya Weimar ilikuwa na matatizo mengi kupita kiasi. Mkataba wa Versailles umefanya mambo mengi kuwa magumu mno kwa uchumi wa Ujerumani. Bajeti ya nchi ikawa hovyo-hovyo. Kulikuwa na matatizo ya kisiasa kwa sababu serikali mara nyingi zilikaa kwa kipindi kifupi sana, na sio kwa kipindi ambacho serikali ingeweza kutoa uamuzi mzuri. Sheria ya uchaguzi ilileta vyama vingi bungeni hivyo haikuwa rahisi kuwa na mapatano ya kuunda serikali.
Kulikuwa na mivutano mingi ya kulia na kushoto. Wafuasi wa utawala wa kifalme na pia wafuasi wa ukomunisti walichukia demokrasia na jamhuri.
Baada ya matatizo ya mwanzoni uchumi uliimarika na jamhuri iliona kipindi cha maendeleo mazuri.
Mambo mazuri ya jamhuri
[hariri | hariri chanzo]Kipindi cha Weimar pia kinafahamika kwa wingi wa utamaduni. Wasanii walio wengi walijaribu kutoa fikra zao mpya na kuweza kutumika hata katika mafilamu. Mtindo wa usanifu wa Bauhaus pia ulianzishwa katika kipindi hicho cha Weimar kunako 1920 hivi.
Kisiasa Ujerumani ilianza kujenga uhusiano mzuri na majirani na kujiunga na Shirikisho la Mataifa.
Mwisho wa jamhuri
[hariri | hariri chanzo]Hali ya uchumi ilirudia kuwa vigumu mno wakati wa kudoda kwa uchumi duanini kuanzia 1929. Idadi ya watu waliokosa kazi ikapanda haraka hadi kufikia milioni sita na umaskini ikaongezeka haraka. Katika chaguzi zilizofuata vyama vya kando kama Chama cha Nazi na Wakomunisti vilianza kupata kura nyingi na vyama vya kidemokrasia vilikosa wabunge wa kutosha.
Kile ambacho sasa tunakiita Jamhuri ya Weimar kimekuja kuwa mwisho wake mnamo tar. 30 Januari ya mwaka wa 1933, pale Adolf Hitler alipokuja kuwa chansela wa Ujerumani.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Constitution of the German Reich (Weimar constitution) of 11th August 1919, in full text Ilihifadhiwa 22 Machi 2021 kwenye Wayback Machine.
- Data Bank
- Documents in German
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Weimar kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |