Nenda kwa yaliyomo

Bauhaus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama ya Bauhaus, mwaka 1922, iliyoundwa na Oskar Schlemmer

Staatliches Bauhaus ilikuwa chuo cha sanaa nchini Ujerumani. Ilianzishwa katika mwaka wa 1919 na Walter Gropius mjini Weimar na kuishi hadi mwaka 1933. Kulingana na vyuo vyingine vya wakati huo, Bauhaus ilikuwa kitu kipya kabisa, tangu  iliunganisha sanaa na ufundi katika mafundisho yake. Bauhaus ni chuo chenye ushawishi mkubwa sana katika uwanja wa usanifu, sanaa na design katika karne ya 20. Leo inaonekana kama makao ya avant-garde ya Classic Modernism katika sanaa na usanifu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Bauhaus ilianzishwa mwaka 1919 kwa kuunganisha Chuo cha sanaa cha Weimar (Großherzoglich-Sächsische Kunstschule Weimar) na Chuo cha ufundi kisanii cha Weimar (Großherzoglich-Sächsische Kunstgewerbeschule Weimar). Mkuu wa kwanza na mwanzishi ni msanifu Walter Gropius. Mwaka 1923 walimu na wanafunzi walifanya maonyesho ya kwanza ya mazao yao, ambayo ni nyumba "Musterhaus am Horn", fanicha, mazulia, na vifaa vya nyumbani aina zote. 1925 Bauhaus iliacha kuishi mjini Weimar na kuendelea kazi yake mjini Dessau. Huko, mwakani 1926, ilijengwa jengo maarufu la Bauhaus, lililoundwa na Walter Gropius. Tena 1930, chuo kililazimishwa kubadili eneo na kwenda Berlin, kilipoachwa mwakani 1933 kwa udhalimu wa serikali ya Adolf Hitler.

Binafsi ushahidi

[hariri | hariri chanzo]