Historia ya Bosnia na Herzegovina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Bosnia na Herzegovina
Eneo la Bosnia na Herzegovina Ulaya

Historia ya Bosnia na Herzegovina inahusu eneo la Ulaya ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Bosnia na Herzegovina.

Bosnia ilitokea kama eneo la pekee wakati wa Karne za kati chini ya utawala wa Dola la Uturuki.

Jina la Bosnia limetokana na mto Bosna, wakati jina la Herzegovina lilitokana na watemi wa kusini katika eneo la mji wa Mostar waliotumia cheo cha Kijerumani cha "Herzog" na eneo lao liliitwa "nchi ya Herzog" au "Herzegovina".

Utawala wa Kiislamu ulisababisha kugeuka kwa sehemu kubwa ya wakazi kuwa Waislamu walioendelea kutumia lugha yao ya Kislavoni.

Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Uturuki katika karne ya 19 utawala wa nchi ulifika mikononi mwa Austria-Hungaria.

Vita kuu ya kwanza ya dunia ilisababishwa mjini Sarayevo kutokana na mauaji ya mfalme mteule wa Austria na mke wake.

Kati ya 1918 na 1992 Bosnia na Herzegovina ilikuwa jimbo la Yugoslavia.

Baada ya uhuru ilitokea vita kali kwa sababu sehemu ya Waserbia na ya Wakroatia walitaka kuunganisha nchi au sehemu zake na Serbia au Kroatia. Wakazi wengi walifukuzwa nyumbani kwao kufuatana na maeneo ambako wanamgambo wa Waserbia au Wakroatia walitawala kufukuza wote wengine.

Jumuiya ya kimataifa iliingilia kati na kuwalazimisha washiriki kukubali amani katika mkataba wa Dayton wa 1995.

Mamlaka kuu haimo mikononi mwa serikali ya wenyeji bali mikononi mwa Kamishna Mkuu kwa Bosnia na Herzegovina anayeteuliwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Ana mamlaka ya kubatilisha sheria zilizoamuliwa na bunge, pia kuachisha mawaziri kazi.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Bosnia na Herzegovina kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.