Historia ya Bulgaria
Historia ya Bulgaria inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Bulgaria.
Historia ya awali
[hariri | hariri chanzo]Zamadamu walikuweko walau miaka milioni 1.4 iliyopita.
Kufikia mwaka 5000 hivi KK kulikuwa na ustaarabu mkubwa uliotengeneza vyombo vya ufinyanzi na usonara vilivyo kati ya vile vya awali zaidi duniani.
Baada ya mwaka 3000 KK, Wathraki walijitokeza katika rasi ya Balkani.
Mwishoni mwa karne ya 6 KK sehemu kubwa ya eneo hilo lilitekwa na Dola la Persia.
Katika miaka ya 470 KK, Wathraki waliunda ufalme wa Odrusia, ambao baadaye ulianguka na wenyewe walitawaliwa na Wamakedonia, Wakelti na Warumi. Mchanganyiko huo wa watu ulikuja kuungana na Waslavi, waliolowea rasi kwa namna ya kudumu baada ya mwaka 500 BK.
Kuunganika chini ya Wabulgaria
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 632 Wabulgaria walianzisha nchi huru kaskazini kwa Bahari Nyeusi iliyoitwa Bulgaria Kuu chini ya Kubrat hadi nusu ya pili ya karne ya 7.
Asparukh, mwandamizi wake, alihamia karibu na delta ya mto Danube akazidi kuteka maeneo ya Balkani yaliyokuwa ya Dola la Bisanti, jambo lililoendelea katika karne zilizofuata.
Huo mchanganyiko mkubwa wa watu ulipata utambulisho wa kitaifa kwa kushika dini, lugha na alfabeti moja.
Katika karne ya 11 hilo dola la Bulgaria la kwanza lilishindwa na Dola la Roma Mashariki likisaidiwa na Warusi.
Lakini mwaka 1185 ndugu Asen na Peter walifaulu kuanzisha dola la pili la Bulgaria lililofikia kilele chake katika miaka ya 1230.
Chini ya Waturuki Waosmani
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kugawanyika, falme tatu za Kibulgaria zilitekwa na Dola la Osmani mwaka 1396 kwa miaka 500 iliyofuata.
Uhuru mpya
[hariri | hariri chanzo]Vita kati ya Urusi na Uturuki vya miaka 1877–1878 vilileta uhuru kwa sehemu ndogo ya Bulgaria. Kwa kutaka Wabulgaria wote wawe ndani yake, nchi iliunga mkono Ujerumani katika vita vikuu vyote viwili na hatimaye ilishindwa.
Hivyo Bulgaria ikawa chini ya Wakomunisti kwa miaka 45.
Baada ya hapo Bulgaria ilijiunga na NATO mwaka 2004 na Umoja wa Ulaya mwaka 2007.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- WWW-VL: History: Bulgaria Ilihifadhiwa 23 Septemba 2017 kwenye Wayback Machine.
- Essential History of Bulgaria in Seven Pages
- History of Bulgaria: Primary Documents
- Historiography in Bulgaria - in Bg
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Bulgaria kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |