Karne ya 6 KK
Mandhari
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ |
Milenia ya 2 KK |
Milenia ya 1 KK |
Milenia ya 1 |
►
◄ |
Karne ya 8 KK |
Karne ya 7 KK |
Karne ya 6 KK |
Karne ya 5 KK |
Karne ya 4 KK |
►
Karne ya 6 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 600 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 501 KK.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- Mashariki ya Kati inatawaliwa kwanza na Babuloni Mpya ya Wakaldayo, halafu na Uajemi uliozidi kuenea hadi kuwa dola kubwa kuliko yote yaliyotangulia.
- Ufalme wa Yuda unakoma mwaka 586 KK, Nebukadneza II alipoteka Yerusalemu na kuhamisha Wayahudi hadi Babuloni. Koreshi Mkuu, mara baada ya kushinda Babuloni, aliwaruhusu kurudi kwao (538 KK).
- Huko Uajemi, Zoroasta anaanzisha dini inayokiri vyanzo viwili vya vyote.
- Zama za chuma barani Ulaya, wanapozidi kuenea Waselti.
- Bahari ya Kati: mwanzo wa falsafa ya Kigiriki.
- Falsafa ya Kichina inakubalika nchini China; Ukonfusio na Utao.
- Gautama Buddha na Mahavira wanaanzisha Ubuddha na Ujain.
- Huko Amerika Kusini, ustaarabu wa Olmec unadumaa.
- 515 KK: Ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu unakamilika: litadumu hadi mwaka 70 BK.
- 510 KK: Wa mwisho kati ya wafalme 7 wa mapokeo ya Roma ya Kale anafukuzwa madarakani; mwanzo wa jamhuri.
Watu muhimu
[hariri | hariri chanzo]- Soloni wa Athene, mtunzi wa Katiba ya Soloni iliyoweka wazi misingi ya demokrasia.
- Pāṇini, huko India, alitunga sarufi ya Kisanskrit, ya zamani kuliko sarufi zote zilizotufikia.[1]
- Nabii Ezekieli, kuhani wa Yerusalemu aliyefanya kazi katika uhamisho wa Babeli.
- Isaya wa pili, nabii kwa Waisraeli wa uhamishoni.
- Nabii Hagai aliyefanya kazi Yerusalemu (520 KK)
- Nabii Zekaria aliyefanya kazi Yerusalemu (520 KK-518 KK)
- Kambise II, mfalme wa Uajemi.
- Dario I, mfalme wa Uajemi.
- Laozi huko China.
- Esopo, mwandishi wa Ugiriki wa Kale.
- Pitagora, mwanafalsafa na mwanahisabati wa Ugiriki wa Kale.
- Heraklito, mwanafalsafa Ugiriki wa Kale.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ritual and mantras: rules without meaning Google Books
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Karne ya 6 KK kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |