Nenda kwa yaliyomo

Ujain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo la Ujain.
Sanamu ya Thirtankara hekaluni

Ujain au Jina Dharma ni dini yenye asili ya Uhindi na wafuasi wake huitwa Wajain. Ilianzishwa mnamo mwaka 500 KK.

Kuna waumini milioni 6 duniani na zaidi ya nusu wako Uhindi.

Wajain hukumbuka walimu 24 wa dini yao wanaoitwa "thirtankara". Thirtankar wa 24 alikuwa Mahavira wakati wa karne ya 6 KK anayetajwa mara nyingi kama mwanzilishi wa dini hiyo, ingawa wenyewe husema hakuna aliyeanzisha hasa.

Kama Ubuddha, hii ni dini isiyo na mafundisho kuhusu Mungu au miungu. Vilevile kama Ubuddha ilianzishwa katika mazingira ya Uhindu wa kale ikikataa matabaka ya kidini jinsi ilivyo katika Uhindu.

Ujain unalenga ukombozi wa nafsi ya binadamu. Kwa ukombozi huu ni muhimu mtu ajifunze kujitawala kwa sababu kila tendo linafuatwa na mazao yake yanayoitwa Karma.

Nafsi katika imani ya Kijain huzaliwa tena na tena katika mwili mpya, kumbe shabaha ni kutozaliwa tena, bali kupata ukombozi na starehe ya milele.

Nafsi au roho haziko ndani ya watu pekee, lakini pia ndani ya wanyama.

Kila tendo linalosababisha mateso kwa kiumbe mwingine linarudisha nafsi katika mzunguko wa kuzaliwa tena. Matendo yanayoharibu karma ya mtu ni hasa mauaji ya viumbe wenye nafsi.

Kwa hiyo Ujain hufundisha kuepukana na uhasama na kutomtenda yeyote kwa mabavu. Kwa sababu hiyo Wajain hukataa kula nyama, kwa kuwa nyama inapatikana kwa njia ya kuua na kutesa wanyama ambao nao ni makazi ya nafsi sawa na wanadamu.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.