Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Slovakia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Slovakia inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Slovakia.

Kwa sehemu kubwa ya historia yake hadi mwaka 1918 Slovakia ilikuwa chini ya watawala wa ukoo wa Habsburg waliokuwa wafalme na makaisari wa Austria.

Baada ya vita vikuu vya kwanza Slovakia ilipata uhuru pamoja na Ucheki katika nchi ya Chekoslovakia, ambayo baada ya vita vikuu vya pili ilitekwa na Wakomunisti.

Baada ya kujikomboa, mwaka 1993 Ucheki na Slovakia ziliachana kwa amani na kuwa kila moja nchi ya pekee.

Slovakia imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Slovakia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.