Nenda kwa yaliyomo

Habsburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Boma la Habsburg katika Uswisi ni nyumba asilia ya nasaba
Simba mwekundu mwenye taji ni nembo la nasaba ya Habsburg
Bendera ya Habsburg ilikuwa pia bendera ya Austria penyewe hadi 1918

Nyumba ya Habsburg ilikuwa nasaba ya watawala wa Austria tangu mwaka 1278 hadi 1918. Kuanzia 1438 hadi 1806 makaisari wa Dola Takatifu la Kiroma walikuwa Wahabsburg isipokuwa katika kipindi cha Kaisari Karolo VII (1742–1745).

Kiasili familia ya Habsburg walikuwa watawala makabaila katika eneo la Aargau (Uswisi). Walifaulu kupanusha eneo lao katika Uswisi uliokuwa sehemu ya Dola Takatifu wakati ule hadi Ujerumani ya Kusini.

Mtemi Rudolf wa Habsburg alifaulu kuchaguliwa kama mfalme wa Wajerumani na mkuu wa Dola Takatifu. Akiwa mfalme aliweza kupata utemi wa Austria na wafuasi walibaki na nafasi hii ya watawala wa Austria.

Mwaka 1438 Mhabsburg mwingine Albert II alichaguliwa tena kuwa mfalme wa Wajerumani. Hakutapata cheo cha Kaisari lakini kuanzia Albrecht wakuu wa Austria walichaguliwa tena kama wafalme wa Wajerumani na wote baada yake walipewa pia taji la Kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma. Tangu 1526 walikuwa pia na cheo cha wafalme wa Hungaria.

Mhabsburg aliyetawala maeneo makubwa kabisa alikuwa Kaisari Karolo V (kama mfalme wa Hispania: Carlos I) (1500 – 1558) aliyeunganisha falme za Dola Takatifu (Ujerumani, Uswisi, Uholanzi, Ubelgiji, Italia Kaskazini, Austria) pamoja na Hispania na koloni zake katika Amerika ya Kati na Amerika Kusini.

Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari Franz II wa Ujerumani alilazimishwa kuacha taji la kaisari la Dola Takatifu lakini alijitanganza kuwa Kaisari Franz I wa Austria akaanzisha cheo cha maikasari wa Austria walioendelea hadi mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia 1918.

Mtawala wa mwisho wa Habsburg alikuwa Karolo I wa Austria (1916-1918) aliyejiuzulu wakati wa kuporomoka kwa milki ya Austria-Hungaria baada ya kushindwa katika vita kuu ya kwanza.

Mwaka 1961 mkuu wa familia Otto von Habsburg alitia sahihi tangazo ya kwamba nasaba yake imeachana na madai yote ya utawala.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Habsburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.