Historia ya Uswidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Uswidi inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Uswidi.

Wakazi wa kwanza kujulikana[hariri | hariri chanzo]

Wakazi hao walikuwa makabila ya Kigermanik kama wakazi wote waliowafuata. Huko Roma Tacitus aliandika juu yao mwaka 98 BK.

Kati ya karne ya 8 hadi ya 11 waliitwa mara nyingi "Waviking" wakiogopwa na wenyeji wa Ulaya bara kwa sababu Waviking walivamia mara kwa mara maeneo ya pwani kwa jahazi zao ndogo. Lakini Waviking au Wanormani ni neno la kutaja watu wa Kaskazini waliovamia na kufanya ujambazi kwenye nchi za Ulaya bara si namna jinsi wenyewe walivyojiita.

Nchi na jirani zake mwaka 1219 BK

Umoja wa Kalmar[hariri | hariri chanzo]

Malkia Margarete I wa Udani aliolewa na mfalme wa Norway. Baada ya kifo cha mumewe alitawala nchi zote mbili na baadaye pia Uswidi. Mwaka 1397 wawakilishi wa falme tatu zilikutana katika mji wa Kalmar (Uswidi ya kusini) na kuelewana juu ya "Umoja wa Kalmar" yaliyounganisha nchi zote za Skandinavia chini ya mfalme wa Denmark ilhali kila nchi iliendelea kujitawala. Wakati ule Ufini (Finland) ilikuwa chini ya Uswidi. Iceland na Visiwa vya Faroe ziliingia pia kwa sababu zilikuwa chini ya Norway wakati ule.

Umoja huo uliendela hadi mwaka 1521. Waswidi walianza kuchoka na utawala wa Kidenmark wakaondoka katika umoja huu mwaka 1521 pamoja na Ufini. Lakini Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka 1814.

Tangu karne ya 16 BK[hariri | hariri chanzo]

Uswidi ulijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kanisa la Kilutheri likawa dini rasmi nchini. Hivyo Uswidi ikawa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri.

Uswidi ulistawi na kueneza himaya yake kuanzia karne ya 17 hadi mwanzo wa karne ya 18 kama mojawapo kati ya nchi zenye nguvu zaidi Ulaya.

Baadaye ilirudi nyuma hadi kunyang'anywa na Warusi Ufini (1809).

Kati ya miaka 1814 na 1905 ililazimisha Norwei kukubali mfalme wa Uswidi kama wake pia.

Tangu hapo Uswidi umeshika msimamo wa amani na wa kutoshikamana na nchi yoyote.

Kwa sasa Uswidi ni ufalme wa kikatiba yaani Mkuu wa Dola ni mfalme (kwa sasa Carl XVI Gustaf), lakini huyu mfalme anapaswa kufuata sheria ya katiba ya nchi. Utawala umo mikononi mwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Katika karne ya 20 Uswidi umefaulu vizuri kujenga uchumi ili kuondoka katika umaskini na kuwa moja kati ya nchi tajiri za dunia (ikiwa na nafasi ya 8 kwa pato la kichwa).

Nchi ilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1995 lakini haikukubali pesa ya Euro ikaendelea na Krona ya Uswidi.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Uswidi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.