Nenda kwa yaliyomo

Visiwa vya Faroe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Føroyar
Færøerne

Visiwa vya Faroe
Bendera ya Visiwa vya Faroe Nembo ya Visiwa vya Faroe
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Tú alfagra land mítt
"We nchi yangu nzuri"
Lokeshen ya Visiwa vya Faroe
Mji mkuu Tórshavn
62°00′ N 06°47′ W
Mji mkubwa nchini Torshavn
Lugha rasmi Kifaroe, Kidenmark
Serikali demokrasia, ufalme wa kikatiba
Mfalme Frederik X wa Denmark
Aksel V. Johannesen
Jimbo la nje la Denmark
Madaraka ya kujitawala

1948
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,399 km² (ya 180)
0.5
Idadi ya watu
 - Desemba 2016 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
49,188 (ya 206)
48,346
35.2/km² (ya 169)
Fedha Krona ya Faroe2 (DKK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC)
EST (UTC+1)
Intaneti TLD .fo
Kodi ya simu +298

-


Ramani ya Visiwa vya Faroe

Visiwa vya Faroe (kwa Kifaroe: Føroyar - "Visiwa vya kondoo") ni funguvisiwa ya Atlantiki ya Kaskazini kati ya Iceland, Uskoti na Norwei.

Historia

Wakazi wa kwanza walikuwa wamonaki kutoka Ireland.

Kati ya miaka 1035 na 1814 visiwa vilikuwa chini ya Norwei. Ndipo vilipotolewa kwa Denmark.

Kufikia mwanzo wa mwaka 1540 wakazi walikuwa wamejiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kuwa Walutheri.

Kuanzia mwaka 1948 ni jimbo la nje la ufalme wa Denmark lenye madaraka ya pekee ya kujitawala. Visiwa vinaendesha shughuli zao isipokuwa siasa ya nje, jeshi na mambo ya mahakama ni chini ya serikali kuu. Hali ya kisiasa ndani ya Denmark inalingana na Greenland ambayo pia ni jimbo la nje la Denmark linalojitawala kwa kiwango kikubwa.

Visiwa vya Faroe viliamua kutoingia katika Umoja wa Ulaya pamoja na Denmark. Kumbe vimeunda umoja wa forodha na Iceland.

Watu

Nyumba za serikali mjini Torshavn.
Feri ikiondoka Torshavn

Wakazi wengi wana asili ya Skandinavia upande wa baba (87%) na ya Wakelti upande wa mama (84%).

Lugha rasmi ni Kifaroe, lugha ya Kigermanik ya Kaskazini karibu na Kiiceland.

Hadi leo 84.1% za wakazi ni Walutheri na madhehebu yao ndiyo dini rasmi.

Uchumi

Uchumi wa visiwa unategemea hasa uvuvi.

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Faroe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.