Feri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kwa ajili ya elementi ya feri tazama chuma
Feri kubwa inayovuka Bahari Baltiki.
Feri mjini Istanbul inayovuka baina Asia na Ulaya
Feri ya kuvukia mto Mbam nchini Kamerun

Kivuko au Feri (ing. "ferry") ni boti au meli inayobeba watu na mizigo kuvuka ziwa, mito na sehemu za bahari.

Kuna feri ndogo zinazohudumia watu wanaoishi mtoni pasipo na daraja. Hapa kuna uwezekano kuendesha feri bila injini kwa kutumia mwendo wa mto mwenyewe. Feri hizi zinahitaji kamba au waya kutoka upande mmoja kwena mwingine.

Feri kubwa zaidi hubeba pia magari na malori pamoja na abiria. Pasipo na madaraja kuna feri za pekee za kubeba treni.

Visiwa maziwani au baharini mara nyingi vinategemea feri kwa mawasiliano na bara. Feri zinapitakana pia kwenye milango ya bahari au kwenye midomo ya hori.

Katika miji inayotumia njia za maji kama Venisi feri ndogo zinafanya kazi kama matatu au basi ya mjini.