Carl XVI Gustaf wa Uswidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Carl XVI Gustav wa Uswidi.

Carl XVI Gustaf wa Uswidi (amezaliwa 30 Aprili 1946) ni mfalme wa Uswidi.

Aliweza kurithi ufalme baada ya babu yake mfalme Gustav VI Adolf kufariki tarehe 15 Septemba 1973. Yeye ni kitinda mimba na mwana wa kiume wa pekee wa Gustaf Adolf kiongozi wa kifalme wa Västerbotten na Sibylla binti wa kifalme wa Saxe-Coburg na Gotha. Baba yake alifariki katika ajali ya ndege nchini Denmaki wakati Carl Gustaf alikuwa na umri wa miezi tisa. Baada ya kifo cha babake, aliweza kuwa mstari wa pili kurithi ufalme wa babu yake, wakati huo akiwa mwana wa kifalme mtarajiwa Gustaf Adolf. Kutokana na kifo cha babu mkubwa wake mfalme Gustaf V mwaka wa 1950, Gustaf Adolf alirithi ufalme na hivyo Carl Gustaf akawa mwana wa kifalme mtarajiwa mpya na mrithi mtarajiwa wa ufalme akiwa na umri wa miaka minne.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carl XVI Gustaf wa Uswidi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.