Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Norwei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Norwei inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Ufalme wa Norwei.

Nchi ilikaliwa na watu wawindaji na wavuvi tangu mwaka 10000 KK hivi.

Katika miaka 3000 - 2500 KK waliingia wakulima wa Kizungu.

Katika karne ya 8 hadi karne ya 10 Norwei ilipeleka mabaharia wake Waviking hadi mbali sana.

Kwa muda mrefu Norwei ilibaki katika muungano na Udani na Uswidi.

Ufalme umekuwa huru tangu mwaka wa 1905.

Sikukuu ya taifa ni tarehe 17 Mei, ambapo husherekewa katiba ya Norwei ya mwaka wa 1814.

Norwei ilikuwa nchi maskini ya wakulima na wavuvi, lakini tangu kupatikana kwa mafuta ya petroli baharini imekuwa kati ya nchi tajiri kabisa duniani.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Norwei kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.