Lugha za Kirumi
Lugha za Kirumi ni lugha zilizotokana na Kilatini kilichokuwa moja kati ya lugha za kale za Kihindi-Kiulaya.
Ni lugha mama kwa watu milioni 800 hivi duniani.
Zimehesabiwa hadi lugha 23 za namna hiyo, ingawa baadhi kwa wengine ni lahaja tu. Tena kuna Krioli nyingi zenye asili katika lugha hizo. Kati ya Krioli hizo, ile ya Haiti na ile ya Shelisheli ni lugha rasmi nchini.
Kilatini cha Roma ya Kale kama lugha mama
[hariri | hariri chanzo]Kilatini kilikuwa lugha rasmi ya utawala, elimu na biashara ya Dola la Roma lililotawala maeneo ya Ulaya ya Kusini, Ulaya ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi kwa miaka mingi, hasa kati ya karne ya 1 KK na karne ya 5 BK.
Kilatini kiliendelea kuwa lugha ya watu wengi katika maeneo mbalimbali ya himaya hii kubwa hasa mijini.
Katika sehemu hizo zilijitokeza lahaja za pekee kulingana na lugha asilia za wenyeji.
Baada ya kuporomoka kwa Dola la Roma la Magharibi, lahaja hizo za Kilatini katika nchi mbalimbali ziliendelea kuchanganyikana na lugha hizo na zile za makabila ya Wagermanik yaliyoteka maeneo hayo yote na hatimaye zikawa lugha za pekee.
Lugha za Kirumi zinazotumiwa kitaifa:
[hariri | hariri chanzo]Lugha ambazo ni muhimi zaidi kama lugha za kitaifa ni:
- Kihispania (milioni 410)
- Kireno (milioni 216)
- Kifaransa (milioni 75)
- Kiitalia (milioni 60)
- Kiromania (milioni 25)
Lugha za Kirumi zinazotumiwa kieneo:
[hariri | hariri chanzo]- Kikatalonia (Català) (Hispania, Ufaransa ya Kusini, Andorra na kwenye visiwa kadhaa za Mediteranea) - wasemaji 8,200,000
- Kigalicia (Galego) (Hispania, jimbo la Galicia) - wasemaji 3,000,000
- Kioksitania (Occitan) (kusini mwa Ufaransa, milima ya Italia ya Kaskazini-Magharibi na bonde la Aran la Hispania)- wasemaji 2,800,000
- Kisardinia (Sardu) (Italia: mkoa wa Sardegna) - wasemaji 1,000,000
- Kiliguria (Lìgure) (Italia ya Kaskazini: mikoa ya Liguria, Piemonte na Sardegna) - wasemaji 500,000
- Kifriuli (Furlan) (Italia Kaskazini-Mashariki: mkoa wa Friuli) - wasemaji 350,000
- Kiladino (Ladin dolomitan) (Italia ya Kaskazini: mikoa ya Trentino-Alto Adige na Veneto) - wasemaji 40.000
- Kirumanj (Rumantsch/Romontsch/Rumauntsch) (Jimbo la Graubünden, Uswisi) - wasemaji 27,000
Lugha za kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Lugha za Kihispania, Kifaransa na Kireno zimesambaa duniani kwa sababu ni lugha kuu za nchi ambazo zilikuwa na makoloni mengi, zikaacha lugha zao katika nchi nyingi, hasa Kihispania ambacho ni lugha kuu ya bara la Amerika, Kireno ambacho ni lugha rasmi ya Brazili na nchi 5 za Afrika na Kifaransa ambacho ni lugha rasmi katika nchi nyingi za Afrika, Amerika visiwani na Kanada.
Kiitalia ni mojawapo ya lugha rasmi za Uswisi, pamoja na nchi ndogondogo za San Marino na Vatikani.
Kiromania ni lugha rasmi ya Moldova pia, ingawa kwa jina la lahaja yake ya Kimoldova.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- Harris, Martin; Vincent, Nigel (1988). The Romance Languages. London: Routledge.
- Posner, Rebecca (1996). The Romance Languages. Cambridge: Cambridge University Press.
- Alkire, Ti; Rosen, Carol (2010). Romance Languages: A Historical Introduction. Cambridge: Cambridge University Press.
Mabadiliko
- Boyd-Bowman, Peter (1980). From Latin to Romance in Sound Charts. Washington, D.C.: Georgetown University Press.
Misamiati
- Holtus, Günter; Metzeltin, Michael; Schmitt, Christian (1988). Lexikon der Romanistischen Linguistik. (LRL, 12 volumes). Tübingen: Niemeyer.
Kifaransa
- Price, Glanville (1971). The French language: present and past. Edward Arnold.
- Kibler, William W. (1984). An introduction to Old French. New York: Modern Language Association of America.
Kireno
- Williams, Edwin B. (1968). From Latin to Portuguese, Historical Phonology and Morphology of the Portuguese Language (tol. la 2nd). University of Pennsylvania.
Kihispania
- Penny, Ralph (2002). A History of the Spanish Language (tol. la 2nd). Cambridge: Cambridge University Press.
- Lapesa, Rafael (1981). Historia de la Lengua Española. Madrid: Editorial Gredos.
- Vicente, Alonso Zamora (1967). Dialectología Española (tol. la 2nd). Madrid: Editorial Gredos.
Kiitalia
- Devoto, Giacomo; Giacomelli, Gabriella (2002). I Dialetti delle Regioni d'Italia (tol. la 3rd). Milano: RCS Libri (Tascabili Bompiani).
- Devoto, Giacomo (1999). Il Linguaggio d'Italia. Milano: RCS Libri (Biblioteca Universale Rizzoli).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Michael de Vaan, Etymological Dictionary of Latin and the other Italic Languages, Brill, 2008, 826pp. (part available freely online) Archived 17 Juni 2013 at the Wayback Machine.
- Lexikon der Romanistischen Linguistik (LRL), edd. Holtus / Metzeltin / Schmitt
- Michael Metzeltin, Las lenguas románicas estándar. Historia de su formación y de su uso, Oviedo, 2004
- Orbis Latinus, site on Romance languages Archived 2 Februari 2011 at the Wayback Machine.
- Hugh Wilkinson's papers on Romance Languages Archived 1 Mei 2011 at the Wayback Machine.
- Spanish is a Romance language, but what does that have to do with the type of romance between lovers? Archived 13 Machi 2013 at the Wayback Machine., dictionary.com
- Comparative Grammar of the Romance Languages
- Comparison of the computer terms in Romance languages Archived 27 Julai 2014 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kirumi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |