Lugha za Kirumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lugha za Kirumi duniani:
buluuKifaransa; kijaniKihispania; machungwaKireno; njanoKiitalia; nyekunduKiromania

Lugha za Kirumi ni lugha zilizotokana na Kilatini cha kale kilichokuwa moja kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Kilatini cha Roma ya Kale kama lugha mama[hariri | hariri chanzo]

Kilatini kilikuwa lugha rasmi ya utawala, elimu na biashara katika Dola la Roma lililotawala maeneo ya Ulaya ya Kusini, Ulaya ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi kwa miaka mingi, hasa kati ya karne ya 1 KK na karne ya 5 BK.

Kilatini kiliendelea kuwa lugha ya watu wengi katika maeneo mbalimbali ya himaya hii kubwa hasa mjini.

Katika sehemu hizo zilijitokeza lahaja za pekee kulingana na lugha asilia za wenyeji. Baada ya kuporomoka kwa Dola la Roma la Magharibi, lahaja hizo za Kilatini katika nchi mbalimbali ziliendelea kuchanganyikana na lugha hizo na zile za makabila ya Kijerumani yaliyoteka maeneo hayo yote na hatimaye zikawa lugha za pekee.

Lugha za Kirumi zinazotumiwa kitaifa:[hariri | hariri chanzo]

Lugha ambazo ni muhimi zaidi kama lugha za kitaifa ni:

Lugha za Kirumi zinazotumiwa kieneo:[hariri | hariri chanzo]

Lugha za kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Lugha za Kihispania, Kifaransa na Kireno zimesambaa duniani kwa sababu ni lugha kuu za nchi ambazo zilikuwa na makoloni mengi zikaacha lugha zao katika nchi nyingi hasa Kihispania ambacho ni lugha kuu ya Amerika, Kireno ambacho ni lugha rasmi ya Brazili na nchi 5 za Afrika na Kifaransa ambacho ni lugha rasmi katika nchi nyingi za Afrika, Amerika visiwani na Kanada.

Kiitalia ni mojawapo ya lugha rasmi za Uswisi, pamoja na nchi ndogondogo za San Marino na Vatikani.

Kiromania ni lugha rasmi ya Moldova pia, ingawa kwa jina la lahaja yake ya Kimoldova.