Nenda kwa yaliyomo

Nagorno-Karabakh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uenezi wa utawala wa Waarmenia katika vita vya Nagorno-Karabakh, 1989-1994.

Nagorno-Karabakh (kwa Kirusi: Нагорный Карабах, yaani Karabakh ya mlimani; kwa Kiazeri: Dağlıq Qarabağ; kwa Kiarmenia: Լեռնային Ղարաբաղ au Արցախ) ni eneo la milima na misitu lisilofikia bahari ndani ya mkoa wa Karabakh, kusini mwa Kaukazi.

Kwa miaka mingi Nagorno-Karabakh iligombaniwa na Armenia na Azerbaijan,[1] na kwa kiasi kikubwa iliunda Jamhuri ya Artsakh ambayo de facto ilijitegemea kwa kuongozwa na wakazi wake wengi wenye asili ya Armenia tangu mwaka 1988 hadi 2023 ilipotekwa moja kwa moja na Azerbaijan.

  1. "General Assembly adopts resolution reaffirming territorial integrity of Azerbaijan, demanding withdrawal of all Armenian forces". United Nations. 14 Machi 2008. Iliwekwa mnamo 30 Ago 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nagorno-Karabakh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.