Nenda kwa yaliyomo

Eneo tegemezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dependent territory)

Eneo tegemezi ni lolote lile ambalo si sehemu kamili ya nchi huru lakini halijapata mamlaka kamili ya kujitawala, bali linategemea dola mlezi kwa viwango tofautitofauti. Hivyo, eneo tegemezi ni tofauti na jimbo au mkoa wa nchi huru kwa sababu si sehemu kamili ya nchi ile. Katika uhusiano na dola mlezi lina uhuru zaidi kuliko majimbo au mikoa yake.

Mara nyingi maeneo tegemezi ni madogo au maskini mno ili kuchukua majukumu yote ya nchi huru pamoja na kujilinda kijeshi na kuwa na mabalozi katika nchi za nje.

Mara nyingi maeneo tegemezi ni mabaki ya makoloni ya awali ambayo wananchi wao hawakupenda kuwa nchi huru wala kuwa sehemu kamili ya nchi tawala ya awali.

Ramani ya maeneo tegemezi duniani
      AUS       CHI       DAN       FRA       NZL       NOR       GBR       USA

Kwa mfano Greenland ilikuwa koloni la Denmark lakini tangu kura ya wananchi mwaka 2009 ni eneo tegemezi la Denmark. Kuna bunge na serikali ya pekee. Ulinzi umo mikononi mwa Denmark, pamoja na sehemu kubwa ya siasa ya nje; Greenland iliamua kutoshiriki katika Umoja wa Ulaya kama ilivyofanya nchi mlezi wake. Ina haki ya kuachana kabisa na Denmark. Hadi sasa sehemu kubwa ya makisio ya serikali yake inatolewa na Denmark.

Mfano mwingine ni eneo dogo la Gibraltar karibu na Hispania ambalo limetawaliwa na Uingereza tangu miaka 300 iliyopita. Eneo lote ni kilomita za mraba 6.7 pekee lenye wakazi 32,000. Hispania inadai Gibraltar kuwa sehemu yake lakini watu wake wamepiga kura mara kadhaa kwa asilimia zaidi ya 90 kuwa wanataka kukaa chini ya ulezi wa Ufalme wa Muungano.

Orodha ya maeneo tegemezi

[hariri | hariri chanzo]

Kuna maeneo tegemezi katika Antaktiki yasiyotambuliwa kimataifa, na haya yanatajwa kwa herufi italiki.

Marekani

[hariri | hariri chanzo]
Tazama pia: Eneo la ng'ambo la Marekani

Marekani ina maeneo tegemezi 11 na madai juu ya maeneo 2. Atolli ya Palmyra katika Pasifiki ni sehemu kamili ya Marekani ila hutawaliwa kama eneo tegemezi kwa sababu haina wakazi. [1]

Bendera Funguvisiwa
au kisiwa
Eneo la nchi kavu
(km²)
Hori la ndani
(km²)
Kifupi cha
ISO 3166-1
Puerto Rico 8.959 -- PR
Visiwa vya Virgin vya Marekani 349 -- VI
Navassa 5,4 --

Kituo cha kijeshi cha Guantanamo kipo pia katika Karibi: ni eneo la Kuba lililokodishwa kwa Marekani.

Visiwa katika Bahari ya Pasifiki

[hariri | hariri chanzo]
Bendera Funguvisiwa
au kisiwa
Eneo la nchi kavu
(km²)
Hori la ndani
(km²)
Kifupi cha
ISO 3166-1
Guam 549 -- GU
Visiwa vya Mariana ya Kaskazini 477 -- MP
Samoa ya Marekani 199 -- AS
Visiwa vidogo vya nje vya Marekani 5,4 -- UM
Kisiwa cha Baker 1,64 --
Kisiwa cha Howland 1,85 --
Kisiwa cha Jarvis 4,50 --
Atolli ya Johnston 2,67 130
Atolli ya Kingman 0,01 100
Atolli ya Midway 6,20 40
Atolli ya Palmyra 3,9 8
Atolli ya Wake 6,50 6

New Zealand

[hariri | hariri chanzo]

New Zealand ina eneo moja tegemezi (Tokelau) na eneo moja ambalo inadai kulitawala huko Antaktiki. Ina pia maeneo mawili (Cook Islands na Niue) yanayojitawala yakiunganishwa nayo kama madola shirikishi.

Norwei ina eneo tegemezi moja pamoja na madai juu ya maeneo mawili mengine.

Ufalme wa Muungano

[hariri | hariri chanzo]
Tazama pia Eneo la ng’ambo la Uingereza

Visiwa vya mfereji wa Kiingereza (Jersey, Guernsey) na Isle of Man si sehemu za Ufalme wa Muungano bali hutazamwa kuwa "maeneo chini ya taji la Uingereza", si chini ya Ufalme wa Muungano.

Ufalme wa Muungano huwa na maeneo tegemezi 13: 10 ya kujitawala, 1 ya kijeshi, 1 bila watu. Kuna pia eneo moja bila watu katika Antaktiki ambako Ufalme wa Muungano unadai ulezi.

Ufaransa

[hariri | hariri chanzo]
Tazama pia: Eneo la ng'ambo la Ufaransa

Ufaransa ilikuwa na makoloni mengi kote duniani. Hadi leo kuna maeneo yaliyo mbali na Ulaya lakini ama yamekuwa sehemu kamili za nchi hiyo au zinasimamiwa kama maeneo tegemezi yaliyopewa hadhi ya “jumuiya ya ng’ambo ya bahari” (collectivite d’outre mer) katika katiba ya Ufaransa ya mwaka 2003.

Maaeneo yote yana wawakilishi katika bunge la Ufaransa na pia katika Bunge la Ulaya. Katika Bunge la Ulaya kuna wawakilishi watatu, mmoja-mmoja kwa maeneo katika Atlantiki, Pasifiki na Bahari Hindi.

Mikoa ya Ng'ambo (Département d'outre-mer) au Jimbo la Ng'ambo (Région d'outre-mer)

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo yafuatayo yanapatikana nje ya Ulaya, yalikuwa makoloni ya Ufaransa lakini wakazi wake walipiga kura kuwa sehemu kamili za Ufaransa zikiwa na hadhi ya mikoa ya ng’ambo au majimbo ya ng’ambo ya Ufaransa. Yote ni pia sehemu kamili za Umoja wa Ulaya.

Hayo ni: Guadeloupe (tangu 1946 - Bahari ya Karibi), Martinique (tangu 1946 - Bahari ya Karibi), Guyana ya Kifaransa (tangu 1946 - Amerika ya Kusini), Réunion (tangu 1946 - Bahari Hindi) na Mayotte katika Bahari Hindi karibu na Komori; mwaka 2011 wakazi walipiga kura wakaamua kuendelea kama Mkoa wa Ng'ambo.

Jumuiya za Kujitawala za Ng'ambo (Collectivité d'outre-mer)

[hariri | hariri chanzo]

Jumuiya hizo zilianzishwa kwa mabadiliko ya katiba ya Ufaransa mwaka 2003. Kila jumuiya imeundwa kwa sheria ya pekee.

Nouvelle-Calédonie au Kaledonia Mpya

[hariri | hariri chanzo]
  • Kaledonia Mpya (katika Pasifiki ya kusini) ni eneo la pekee; wakazi walijadili uhuru lakini waliamua kwa kura ya mwaka 2018 kubaki kama jumuiya chini ya Ufaransa.

Visiwa visivyokaliwa na watu

[hariri | hariri chanzo]

Ufaransa hutawala au kudai utawala juu ya visiwa vidogovidogo bila wakazi:

Visiwa vya kusini na eneo la Antaktiki (Terres australes et antarctiques françaises)

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo hayo yanatawaliwa kutoka Réunion. Hakuna wakazi wa kudumu, hivyo ni maeneo ya pekee yasiyo na haki za kisiasa: kuna visiwa vya Amsterdam, Saint-Paul, Crozet, Kerguelen na eneo la Adélieland kwenye Antaktiki, halafu Îles Éparses.

Visiwa hivyo hudaiwa pia na Madagaska na Tromelin inadaiwa na Shelisheli.

  1. "Definitions of Insular Area Political Organizations". U.S. Department of the Interior. Iliwekwa mnamo 6 Aprili 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)