Visiwa vya Cook
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Te Atua Mou E Mungu ni Ukweli | |||||
Mji mkuu | Avarua | ||||
Mji mkubwa nchini | Avarua | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza Kimaori | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Charles III wa Uingereza Tom Marsters Mark Brown | ||||
Uhuru Kujitawala kwa ushirikano wa hiari na New Zealand |
4 Agosti 1965 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
240 km² (ya 209) -- | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 2021 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 223) 15,040 66/km² (ya 138) | ||||
Fedha | Dollar ya New Zealand (pia Dollar ya Cook Islands) ( NZD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-10) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .ck | ||||
Kodi ya simu | +682
- |
Visiwa vya Cook (kwa Kiingereza: Cook Islands, kwa Kimaori: Kūki 'Āirani) ni nchi huru ya Polynesia katika Pasifiki iliyopo katika hali ya ushirikiano wa hiari na Nyuzilandi.
Eneo lake ni visiwa vidogo 15 vyenye eneo la km² 240.
Mji mkuu wa Avarua uko kwenye kisiwa cha Rarotonga.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Jina limetolewa kwa kumbukumbu ya mpelelezi Mwingereza James Cook aliyefika kwenye kisiwa cha Manuae mwaka 1773 na kuchora visiwa hivi mara ya kwanza kwenye ramani ya dunia.
Visiwa vilikuwa eneo lindwa la Uingereza katika karne ya 19 kufuatana na ombi la malkia wa Cook aliyeogopa uvamizi wa Ufaransa wakati ule.
Chini ya utawala wa Kiingereza viliwekwa chini ya usimamizi wa serikali ya New Zealand, zikabaki hivyo katika hatua mbalimbali za uhuru wa New Zealand.
Mwaka 1965 New Zealand ikawapa watu wa Cook nafasi ya kujiamulia kuhusu uhuru wao. Visiwa viliamua kujitawala katika ushirikiano na New Zealand. Hatua hiyo ilisimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa azimio lake No. 1514 (XV).
Sheria huamuliwa na bunge la visiwa vya Cook. Serikali haisimamiwi na New Zealand. Wananchi wote wana uraia wa New Zealand inayoendesha pia shughuli za jeshi na siasa ya nje kwa niaba ya visiwa. Visiwa vya Cook vimebaki na nafasi ya kufanya mapatano na nchi za nje vilevile.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Wakazi ni 15,040 (2021), karibu wote wenye asili ya Kimaori (78.2%) na machotara wa Kimaori (7.6%).
Lugha zinazotumika ni hasa Kiingereza (86.4%) na Kimaori (76.2%).
Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti (68.2%) na Wakatoliki (17%).
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Utalii ni biashara kuu visiwani.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mwambao wa Rarotonga
-
Kisiwani Aitutaki
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Cook Islands, the best kept secret in the Pacific Ocean - The Most Comprehensive Website
- Cook Islands - Detailed and non-commercial website
- Cook Islands Government Ilihifadhiwa 21 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- Cook Islands Government (summary)
- Cook Islands Tourism Corporation
- Open Directory Project - Cook Islands directory category
- Cook Islands National Environment Service Ilihifadhiwa 15 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Cook Islands Biodiversity Database
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|